IQNA

Spika wa Bunge la Iraq

Umma wa Kiislamu unakabiliwa na hatari ya wenye misimamo mikali

17:30 - October 22, 2016
Habari ID: 3470628
Spika wa Bunge la Iraq amesema Umma wa Kiislamu unakabiliwa na hatari kubwa kutokana na makundi ya wenye misimamo mikali nay a kufurutu ada.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Salim Abdullah al-Jabouri Spika wa Bunge la Iraq ameyasema hayo leo Jumamosi mjini Baghdad alipohutubu katika kikao cha ufunguzi wa Kongamano la 10 ya Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu.

Al Jabouri ameongeza kuwa, mkutano huo ni fursa ya kweli kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbali mbali ya umma wa Kiislamu. Aidha ametoa wito kwa nchi zinazopakana na Iraq, hasa Iran, Uturuki na Saudi Arabia kuitisha kikao cha pamoja kwa lengo la kujadili njia za kufikia usalama na maelewano ya kudumu katika eneo.

Ameongeza kuwa: "Katika kipindi chote cha miaka 1400, umma wa Kiislamu umekuwa ukitegemea wasomi, wanasayansi na wanazuoni katika hali ambayo hivi leo Ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na hatari ya watu wenye misimamo mikali na ya kufurutu ada huku magaidi wakijaribu kutumia jina la Uislamu kueneza itikadi yao potofu.

Spika wa Bunge la Iraq pia amesema wote duniani wana jukumu la kukabuluana na idiolojia ya misimamo mikali na kwamba suala hilo linahitaji mpango kami wenye kuwashirikisha wasomi na wanafikra.

Mkutano huo pia umehudhuriwa pia na Heidar al Abadi Waziri Mkuu wa Iraq, Sayyid Ammar Hakum Mkuuwa Muungano wa Kitaifa wa Iraq na Ali Akbar Velayati Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu.

Mkutano huo unafanyika chini ya kaulimbiu ya, "Iraq, sote kwa pamoja katika kufikia umoja na kuvunja njama za wakufurishaji na magaidi."

3539740

captcha