IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Bosnia

12:31 - November 29, 2015
Habari ID: 3458214
Duru ya 10 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Bosnia na Herzegovina yamefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Sarajevo.

Kwa mujibu wa tovuti ya tafsir.net, mashindano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani (HQMI) kwa ushirikiano na Taasisi ya Kiislamu na Kuhifadhi Qur'ani Bosnia.
Mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti wa Gazi-Husrev-bey mjini Sarajevo ambapo kulikuwa na washiriki 53 wa kike na kiume.
Mashindano hayo yalikuwa na kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na pia kuhifadhi Juzuu 15 na tano.
Walioshika nafasi za juu walitunukiwa zawadi katika hafla iliyohudhuriwa na wasomi wa Qur'ani, Sheikh Hussein Samovich aliyewakilisha wanazuoni wa Kiislamu, Muhammad Ayat Mansour Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani na Nusrat Abdi Begovic mkurugenzi wa Elimu na Miongozo ya Kidini katika Kituo cha Kiislamu cha Bosnia.
Msikiti wa Gazi Husrev-bey ulijengwa karne ya 16 Miladia na ni mkubwa zaidi wa kihistoria Bosnia na Herzegovina ambao pia hutumika kama msikitu mkuu  wa jamaa katika nchi hiyo ya Waislamu kusini mwa Ulaya.

3458106

captcha