IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Wasimamizi wa Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran kuwaenzi watumishi wa Qur'ani

15:50 - March 26, 2024
Habari ID: 3478585
IQNA - Hafla itafanyika katika toleo la 31 la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kuwaenzi wanaharakati na watumishi kadhaa mashujaa wa Qur'ani na wengine wanaotumikia Kitabu Kitukufu.

Kongamano la 29 la Kuwaenzi Watumishi wa Qur'ani litaandaliwa Katikati ya Ramadhani kama miaka iliyopita.

Alisema Rais wa Iran, Sayyid Ebrahim Raeisi anatazamiwa kushiriki katika hafla hiyo.

Mwaka huu, watumishi 13 wa Qur'ani  wamechaguliwa ambao wataheshimiwa katika sherehe inayokuja, alibainisha.

Wanafanya kazi katika nyanja tofauti zinazohusiana na Qur'ani Tukufu, Sarabi aliendelea kusema.

Takriban watu 300 wakongwe wa Qur'ani wametunukiwa katika matoleo yaliyopita.

Kuna mapendekezo kwamba watumishi wa Quran kutoka nchi nyingine pia waenziwe katika siku zijazo.

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa Jumatano Machi 20 katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA) na yanaendelea kwa muda wa wiki mbili.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

3487718

 

Habari zinazohusiana
captcha