IQNA

Qurani Tukufu

Msikiti mkubwa uliofadhiliwa na wenyeji wazinduliwa Wallonia Ubelgiji

15:57 - March 13, 2024
Habari ID: 3478503
IQNA - Eneo la Wallonia nchini Ubelgiji linasherehekea ufunguzi wa Msikiti wa Kanuni Sultan Süleyman huko Liège baada ya miaka 10 ya ujenzi uliotegemea wafadhili wa eneo hilo.

Msikiti huo ni matokeo ya mpango wa muongo mmoja wa michango ya wenyeji wa eneo hilo ambapo, Euro milioni 4.5 zilikusanywa bila msaada wowote wa kifedha wa serikali au wa kigeni.

Ukiwa na mita za mraba 1,300, jengo jeupe la kisasa la msikiti huo una ukumbi mkuu wa Sala wenye ukubwa wa mita za mraba 450 lililo na kuba.

Tofauti na miundo ya jadi, msikiti hauna minara bado unaweza kuchukua hadi waabudu 600.

Mehmet Aydogdu, Mwakilishi wa Masuala ya Kitamaduni wa Liège, amebaini fikra iliyopelekea kuwepo usanifu majengo wa kipekee wa msikiti huo kwa kusema: "Wazo letu halikuwa kufanya usanifu majengo kuhusiana na Anatolia ya Kati, Mashariki ya Kati au Afrika Kaskazini bali lilikuwa kufikia ulimwengu wote."

Msikiti huo umejengwa katika eneo ambalo lilikuwa na mgodi wa makaa ya mawe ambalo lilishuhudia mawimbi ya wachimba migodi wa Kituruki waliofika eneo hilo muongo wa sitini.

Imam Ertugrul Yilmaz, mzaliwa wa Wallonia ambaye baadaye alisoma nchini Uturuki, alionyesha uhusiano wake wa kina na jamii: "Ni fahari kubwa kwangu kurudi, kuwa imamu, kwa sababu nilikua nao. Ninawajua, wananijua. Tunaweza kufanya kazi pamoja.

"Tungependa kukaribisha kila mtu ili kuonyesha kwamba tunaishi pamoja, kwamba sisi pia ni Wabelgiji, kwamba sisi ni sehemu ya jumuiya hii."

Zaidi ya jukumu lake kama mahali pa ibada, jumba la msikiti linajumuisha kituo cha kitamaduni kinachoweza kutumiwa  watu wa dini zote, kinachohudumia matukio mbalimbali kama vile mikutano, programu za elimu na shughuli za jumuiya, na kukuza zaidi mazungumzo na maelewano miongoni mwa jamii mbalimbali.

3487551

Kishikizo: msikiti ubelgiji
captcha