IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Meya wa Arnhem, Uholanzi atoa wito wa kupigwa marufuku kuvunjiwa heshima Qur'ani

11:35 - January 26, 2024
Habari ID: 3478255
IQNA - Meya wa mji wa Arnhem nchini Uholanzi Ahmed Marcouch aliwataka wanasiasa wa kitaifa kuharamisha vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, huku akisema vitendo hivyo ni "vya sumu vinavyowakera wengine".

Alitoa kauli hiyo siku ya Jumatano wakati wa mjadala wa baraza la jiji, kufuatia kufeli tukio la kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ambalo lilikuwa limepangwa na kundi linalopinga Uislamu la Pegida huko Arnhem mnamo Januari 13.

Kiongozi wa Pegida Edwin Wagensveld alijaribu kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu huko Arnhem, lakini aluzuiwa na wapinzani, wengi wao wakiwa Waislamu. Ghasi zilizoibuka hapo zilisababisha watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kukamatwa.

Marcouch alisema ana wasiwasi kuhusu "mgawanyiko wenye sumu" unaosababishwa na vitendo kama hivyo, na akaomba kuheshimiwa zaidi kwa maoni na imani tofauti.

Pia alisema kuchoma vitabu vitakatifu kunaweza kuhatarisha usalama wa taifa, kwani kunaweza kuzua hisia kali kutoka nje ya nchi. Alisema alikuwa akiwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje kabla na baada ya tukio hilo huko Arnhem.

"Natamani sheria ingeturuhusu kutomuona tena mtu huyu wa Pegida akijitokeza kama mchomaji nakala ya Qur'ani huko Arnhem tena," alisema.

Wakati huo huo, Pegida ilitangaza Jumatano kwamba inapanga kuandaa uchomaji mwingine wa nakala ya Qur'ani Tukufu huko Arnhem mwishoni mwa Machi.

Wagensveld ana historia ya matukio ya uchomaji wa Qur'ani Tukufu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Alichoma au kurarua nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya jengo la muda la bunge la Uholanzi huko The Hague na katika maandamano ya peke yake huko Utrecht mnamo 2022 na 2023. Pia alikamatwa huko Rotterdam na The Hague kwa kujaribu kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu bila kuzingatia sheria za maandamano. Katika visa vyote viwili, vikundi vya Waislamu vilifanya maandamano ya kupinga vitendo vya Pegida. Mwaka jana, Wagensveld pia alirarua nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya Ubalozi wa Uturuki huko The Hague.

3486958

captcha