IQNA

Elimu ya Qur'ani Tukufu

Kongamano la Kimataifa la Sayansi ya Qur'ani Lamalizika nchini Libya

13:59 - December 11, 2023
Habari ID: 3478020
IQNA - Libya imeandaa kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu sayansi ya Qur'ani Tukufu.

Kitivo cha fasihi cha Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Saied Mohamed Bin Ali Al Sanussi kiliandaa hafla hiyo mnamo Desemba 6-8, kulingana na tovuti ya Al-Wasat.

Wanazuoni na watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu waliwasilisha makala kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza kuhusu ufasaha wa Qur'ani na vipengele vyake vya lugha.

Kusonga mbele katika kusoma vizuri zaidi Balagha (ufasaha) na isimu ndiyo ilikuwa mada ya mkutano huo.

Pia mkutano huo ulimuangazia na kumuenzi mwanachuoni wa Qur'ani Tukufu Mohammad Tayyib Khatib kwa huduma na juhudi zake za kukuza lugha ya Kiarabu na sayansi ya Qur'ani Tukufu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na juhudi nyingi katika nchi za Kiislamu za kukuza sayansi za Qur'ani hasa zinazohusu lugha ya Kitabu hicho Kitukufu.

captcha