IQNA

Wanamichezo Waislamu

Nyota wa soka wa Ufaransa: Uislamu ulibadilisha maisha yangu

20:14 - September 16, 2023
Habari ID: 3477608
PARIS (IQNA)- Katika mahojiano kwenye televisheni, Paul Pogba, mchezaji wa soka wa Ufaransa na klabu ya Juventus ya Italia, alijadili sababu zilizomfanya kusilimu na jinsi hatua hiyo ya kuukumbatia Uislamu ilivyoathiri maisha yake.

 

Katika mahojiano, Pogba, alieleza sababu iliyomfanya kusilimu na athari za Uislamu katika maisha yake.

Katika mahojiano na Al Jazeera Generation Sport, Pogba alizungumzia mabadiliko makubwa aliyoyapata baada ya kusilimu.

Mchezaji huyu wa Ufaransa alieleza sababu iliyomfanya kusilimu: “Nilisali mara moja na nikahisi moyo wangu umeyeyuka na kana kwamba mwili wangu umepata uhai mpya, nikasema akilini mwangu hii ni dini yangu. Niliujua Uislamu kusilimu baada ya kukutana na marafiki zangu Waislamu.

Pogba alibainisha kuwa marafiki zake Waislamu walimshawishi kwa maadili yao, mtindo wa maisha na mazoea ya kiroho.

Nyota huyu wa soka wa Ufaransa alisisitiza kwamba: "Ikiwa nitamtii Allah SWT basi daima nitapata mafanikio. Kabla ya Uislamu, maisha yangu yalihusiana na soka, lakini baada ya hapo, mawazo yangu kuhusu maanda kushinda na kushindwa yamebadilika. ."

Akaendelea kusema: Mabadiliko makubwa ambayo Uislamu umefanya katika tabia yangu ni subira. Uislamu umenifundisha nisikasirike jambo baya linapotokea.

Pogba alihitimisha kwa kusema: "Pesa hubadilisha watu na inaweza kuharibu familia na kuanzisha vita. Wakati mwingine mimi hujiambia: Sitaki pesa zaidi au sitacheza mpira wa miguu tena. Nataka kuwa mtu wa kawaida na kuishi na watu wa kawaida. Wale wanaonipenda kwa ajili yangu, si kwa sababu ya pesa. Nyakati fulani hali ilikuwa ngumu, lakini Mwenyezi Mungu alinisaidia kushinda mawazo hayo na kupata nguvu za kuendelea.

4169061

captcha