IQNA

TEHRAN (IQNA) – Duru ya 10 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Libya imeanza Jumapili katika mji wa Benghazi.

17:54 - June 14, 2022
Habari ID: 3475376
TEHRAN (IQNA) – Duru ya 10 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Libya imeanza Jumapili katika mji wa Benghazi.

Wawakilishi wa nchi 40 wanashiriki katika mashindano hayo ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Qur'ani na  Sunnah ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Libya.

Mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani yanafanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 tokea nchi hiyo itumbukia katika vita  vya ndani.

Libya ni nchi ya Kiislamu kaskazini mwa Afrika na ina karibu watu milioni moja waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

4064084

captcha