IQNA

Rais wa Iran awatumia salamu za Idul Fitr viongozi wa nchi za Kiislamu

7:12 - May 24, 2020
Habari ID: 3472795
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia viongozi wa nchi za Kiislamu na Waislamu kote duniani salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia siku kuu ya Idul Fitr.

Katika ujumbe wake huo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea matumaini yake kuwa, kwa baraka za Idul Fitr na kutokana na jitihada za wasomi na wataalamu, watu wa dunia wataweza kukabiliana kwa mafanikio na changamoto, masaibu na matatizo ambayo yamemkumba mwanadamu hasa kirusi cha corona. Aidha rais wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa, kara baraka za Idul Fitr kutapatikana afya, amani, usalama na utulivu katika jamii za Waislamu na watu wote kwa ujumla duniani.

Naye Ali Larijani spika anayeondoka wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), pia amewatumia maspika wa mabunge ya nchi za Kiislamu salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia siku kuu ya Idul Fitr.  Larijani amesema katika dunia ya sasa, nafasi ya mabunge ya Kiislamu ni muhimu katika kukabiliana na changamoto katika ulimwengu wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na janga la corona.

Jumapili Mei 24  sawa na Shawwal Mosi ni siku kuu ya Idul Fitr katika aghalabu ya nchi za Kiislamu duniani .

115480

captcha