IQNA

Nchi 20 zashiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Tanzania

20:36 - November 27, 2017
Habari ID: 3471282
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yamefanyika siku chache zilizopita nchini Tanzania na kushirikisha nchi 20.

Mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa Kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zilihudhuriwa na wageni kadhaa waheshimiwa akiwamo rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakr bin Zubair bin Ali na mabalozi wan chi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu walioko Tanzania.

Washindi katika mashindano hayo walitunukiwa zawadi huku Abdullah Basfar, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani akitunukiwa zawadi kama Shakhsia wa Qur’ani katika mwaka huu.

3667008

captcha