IQNA

Mkutano wa 8 wa Radio na Televisheni za Kiislamu waanza Tehran

21:07 - August 16, 2015
Habari ID: 3344930
Kikao cha Nane cha Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu kimeanza leo hapa mjini Tehran.

Kongamano hilo limeanza kwa hotuba ya Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Kimataifa Ali Akbar Velayati na Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Karimian Katibu Mkuu wa Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu.
Karimian amesema kaulimbiu ya kikao hicho cha siku mbili itakuwa: ‘Mtume wa Rehema (saw), Ujumbe wa Vyombo vya Habari vya Mapambano.’ Pia amesema kuwa shirika la habar la UNEWS litazinduliwa kwenye kikao hicho jukumu lake kuu likiwa ni kuwezesha ubadilishanaji habari kati ya vyombo vya habari vya muungano huo.
Ameongeza mkutano huo utakuwa pia na maonyesho ya mafanikio na ustawi katika sekta ya habari na mawasiliano na pia maonyesho ya filamu 800 zilizotengenezwa na vyombo vya habari vya Kiislamu. Aidha katiak kikao cha mwaka huu kinajumuisha kuzinduliwa  Idara ya Kutoa Cheti cha Vyombo vya Habari Halali.../mh

3344605

captcha