IQNA

Kombe la Dunia Qatar

Mtaalamu: Qatar imeweza kubatilisha taswira potovu ya Magharibi kuhusu Uislamu

17:55 - November 30, 2022
Habari ID: 3476176
TEHRAN (IQNA) - Mtaalamu mmoja anasema maandalizi "ya kuvutia" ya Qatar ya Kombe la Dunia la FIFA la 2022 yamebatilisha juhudi za nchi za Magharibi za kuonyesha picha mbaya ya Waislamu na Waarabu ambapo daima wamekuwa wakihusishwa na ugaidi na machafuko.

Mabilioni kote ulimwenguni wanatazama Kombe la Dunia la FIFA la 2022 ambalo kwa mara ya kwanza linaandaliwa na nchi ya Kiislamu.

Ili kuangazia zaidi ukosoaji wa vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya Qatar, IQNA imewasiliana na Abdennour Toumi, mtaalam wa masomo wa Afrika Kaskazini katika Kituo cha ORSAM (Kituo cha Mafunzo ya Mashariki ya Kati) nchini Uturuki.

Katika mahojiano na IQNA, amesema, "Ukosoaji huu "usio wa haki" dhidi ya Qatar unaofanywa na nchi za Magharibi "umeonyesha kiburi na pia kutoelewa madhumuni ya tukio hili."

Kandanda si mchezo wa kawaida tu kwa watu maskini, alisema, akibainisha kuwa imekuwa ni hitaji kubwa la kiuchumi la kijiografia na kisiasa katika jukwaa la dunia.

Akijibu swali kuhusu jinsi namna mipango ya Qatar ya kutambulisha Uislamu inaweza kuongeza ufahamu kuhusu dini hii tukufu na kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, mtaalamu huyo aliipongeza Doha kwa "kuonyesha maadili ya ulimwengu wa Kiislamu."

"Hatulegezi msimamo juu ya maadili yetu na Qatar imefanikiwa katika hilo," alisema.

Toumi alibainisha Wamagharibi wakiwa  wanachochewa na "kiburi kisichoeleweka na bado wangali wanawatazama watu wa nchi zingine duniani kama watumwa wao."

Mtaalamu huyo alisisitiza kwamba nchi za Magharibi haziwezi "kulazimisha" maadili yao potovu  kama "maadili ya jumla" kwa ubinadamu wote.

"Madola ya magharibi yamekuwa yakieneza taswira potovu kuhusu Waislamu," alisema, akiongeza kwamba siku zote wanajaribu kuwahusisha Waarabu na ugaidi na machafuko. Halikadhalika  amesema madola ya Magharibi hayataki kuona ustaarabu katika Mashariki ya Kati.

"Waislamu wanajivunia sana kile ambacho Qatar imefanya," aliongeza.

Ukosoaji huo ungekuwepo hata kama Kombe la Dunia lingeandaliwa Iran, Saudi Arabia, Morocco, Algeria na Tunisia, mtaalamu huyo alibainisha.

Alipoulizwa kuhusu katuni ya matusi kwenye jarida la Ufaransa kuhusu uenyeji wa Qatar wa Kombe la Dunia, mtaalamu huyo alisema hii inaendana na "hisia za chuki dhidi ya Waarabu na Waislamu" nchini Ufaransa na imekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Ufaransa hivi majuzi ilishuhudia jinsi vuguvugu la mrengo wa kulia lilivyotumia hisia hizi kupata kura nyingi katika uchaguzi huo, aliongeza.

Pia kuna hisia dhidi ya Qatar nchini Ufaransa baada ya Mqatari kununua PSG na kuonyesha "usimamizi mzuri wa timu," alidokeza.

3481462

captcha