IQNA

Ukweli katika Qur'ani Tukufu / 7

Kuna uhusiano upi baina ya dini uvumilivu au istiqama

16:08 - November 29, 2022
Habari ID: 3476167
TEHRAN (IQNA)- Maisha ya watu yamejaa changamoto na magumu yasiyotarajiwa. Kila mtu, kwa kuzingatia hali na hadhi yake, hukabiliana na matatizo au masaibu mbalimbali ya kibinafsi, ya kifamilia na kijamii lakini si watu wote wanaoyavumilia na kuyastahimili vivyo hivyo.

Hisia hasi, ambazo ni kati ya hisia kuu tunazokabiliana nazo maishani, huweka gharama kubwa kwa watu binafsi na familia kote ulimwenguni. Huzuni, dhiki, wasiwasi na mfadhaiko wa akili ni baadhi ya hisia hasi.

Kuhusu ni nini husababisha hisia kama hizo, inapaswa kusemwa kwamba sisi sote tuna maoni sawa tunapokabiliana na matukio mabaya. Kwa mfano tunahuzunika tunapopoteza kitu au mtu fulani na huzuni hii inaweza kukua na kuwa kubwa sana hivi kwamba inaweza kuathiri maisha na mwenendo wetu.

Wakati mwingine hofu hutawala maisha yetu au tunakua na wasiwasi wa kutofikia malengo yetu maishani. Au pengine wengine wanakanyaga haki zetu na kutufanya tuhuzunike na kukasirika.

Hatuwezi kuishi bila matatizo na changamoto. Hata watu wetu wa karibu kifamilia au kiukoo wanaweza kufanya mambo ambayo hatukutazamia na kuyaona kuwa hayapendezi. Huu ni ukweli wa maisha kwamba huzuni na mateso ni sehemu ya maisha yetu na hayawezi kuondolewa kabisa. Pia ni ukweli kwamba huzuni kawaida huchukua muda mrefu na furaha ni ya muda mfupi. Hii ndiyo asili ya maisha.

Kulingana na tafiti zilizofanywa na wanasaikolojia, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya afya ya kisaikolojia na maadili. Maadili hutuambia ni kiasi gani tunaweza kuvumilia maumivu ya kisaikolojia na huzuni. Kwa hiyo kiwango cha kuvumilia na kustahimili matatizo na magumu kinategemea mfumo wetu wa thamani. Ndiyo maana wanasaikolojia wanajaribu kuongeza kiwango cha uvumilivu cha watu dhidi ya matatizo na masaibu kwa kuimarisha thamani ya msingi.

Uhusiano kati ya afya ya kisaikolojia na dini na uhusiano na Mwenyezi Mungu ni muhimu sana hapa. Ikiwa uhusiano huu ni thabiti, mtu atakuwa na nguvu katika kustahamili shida. Pia, uhusiano wa mtu pamoja na Mwenyezi Mungu humpa tumaini na kumsaidia kutoka katika huzuni kwa urahisi zaidi.

Suala lingine muhimu ni kudharau mambo ambayo husababisha huzuni, na mafadhaiko. Mojawapo ya mambo haya ni Shetani na mawazo maovu yanayopenya mioyoni mwetu. Tunapokuwa na huzuni na kufadhaika, uhusiano wetu na Mungu hudhoofika na chini ya hali kama hizo, njia hufunguka kwa ajili ya kujipenyeza kwa Shetani. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani Tukufu:

“Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (Surah al-Baqarah, Aya ya 268)

captcha