Qur'ani Tukufu ina mifano miwili kuhusu motisha au nia zisizo sahihi katika kutoa sadaka ambapo inaonyesha jinsi tabia kama hiyo ilivyo mbaya na isiyo na maana.
Mojawapo ya mienendo mikuu ya kimaadili katika jamii inayochochewa na waja wema kuwasaidia wenye uhitaji kwa njia mbalimbali. Hata hivyo, kama misaada hii haitatolewa kwa njia sahihi, sio tu kwamba haitakuwa na athari chanya za kijamii bali malipo ya amali njema huko akhera pia yanaweza kubatilishwa.
Qur'ani Tukufu ina ushauri mwingi kuhusu hili, ukiwemo ule ulio katika aya ya 264 ya Surah Al-Baqarah:
“ Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.”
Tafsiri ya Nemouneh wa Qur'ani Tukufu inasisitiza kwamba katika aya hii, Qur'ani Tukufu inatumia mifano miwili kuonyesha jinsi tabia mbaya inavyofanya kutoa sadaka kutokuwa na thamani na ubatili.
Mfano wa kwanza ni: “(Mtu huyo) ni kama anayetoa mali yake kwa ajili ya kujionyesha kwa watu na hamwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho.”
Mfano unaofuata ambao Quran inaitaja ni huu: “Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.”
Hivyo vitendo hivyo vinavyohusisha unafiki, lawama na maudhi hutoka katika mioyo migumu na watu wa aina hiyo hawanufaiki navyo.
Ujumbe wa aya kwa mtazamo wa Tafsiri ya Noor ya Qur'ani Tukufu: