IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza katika mji mkuu wa Urusi

16:55 - November 19, 2022
Habari ID: 3476115
TEHRAN (IQNA) –Mashindano ya 20 Kimataifa ya Qur'ani ya Moscow yalizinduliwa Ijumaa katika mji mkuu huo wa Urusi (Russia).

Baraza la Mufti la Russia limeandaa mashindano hayo kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu.

Msikiti Mkuu wa Moscow ni mwenyeji wa hafla hiyo ya kimataifa ambayo katika sherehe za ufunguzi imehutubiwa na Sheikh Rushan Abbyasov, naibu mwenyekiti wa Baraza la Mamufti wa Urusi, kwa niaba ya rais wa baraza hilo Sheikh Rawil Gaynutdin. Msomi huyo wa Kiislamu aliwakaribisha washiriki na kusema kuandaa mashindano hayo ni heshima kubwa kwa Moscow.

Alielezea kufurahishwa kuona mashindano hayo yanafanyika tena baada ya kusimama kwa miaka miwili kutokana na janga la corona.

Aidha amesema yeyote anayeshiriki katika mashindano hayo ni mshindi kwa baraka za Qur'ani Tukufu bila kujali matokeo.

Kulingana na Sheikh Ismail Gundulin, mratibu wa kamati ya maandalizi, wawakilishi wa nchi 21 wanashiriki katika tukio la mwaka huu.

Qari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Mostafa Hosseini atakuwa mshindani wa 17 kuonesha vipaji vyake vya usomaji Qur'ani katika mashindano hayo.

Kuwait, Iraq, Tajikistan, Uzbekistan, Lebanon, Falme za Kiarabu, Sudan, Misri, Morocco, Kazakhstan, Syria, Tanzania, Bangladesh na Yemen ni miongoni mwa nchi nyingine zinazoshiriki katika hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani.

Wajumbe wa jopo la waamuzi ni wataalamu wa Qur'ani kutoka Yemen, Uturuki, Lebanon, Russia na Saudi Arabia.

Mashindano hayo yataendeshwa katika mji mkuu wa Urusi hadi Jumatatu, kulingana na waandaaji.

Int’l Quran Contest Kicks Off in Russian Capital  

Int’l Quran Contest Kicks Off in Russian Capital  

Int’l Quran Contest Kicks Off in Russian Capital  

Int’l Quran Contest Kicks Off in Russian Capital  

Int’l Quran Contest Kicks Off in Russian Capital  

 

4100631

captcha