Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha BFMTV cha Ufaransa, Le Pen amesema kuwa Darmanin "anafunga msikiti hapa na msikiti pale... Ni lazima afunge misikiti yote yenye itikadi kali katika ardhi zetu." Amesisitiza haja ya kuwafukuza nchini Ufaransa Waislamu wote ambao amedai wanafuata matamshi ya itikadi kali.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, serikali ya Ufaransa imefunga misikiti 24 kati ya 99 ambayo imefuatiliwa kwa kisingizio cha "kupambana na itikadi kali".
Taratibu za kisheria bado zinaendelea kwa ajili ya kufunga misikiti mingi zaidi ya Waislamu kwa ombi la Waziri wa Mambo ya Ndani wa ufaransa.
Marine Le Pen ambaye alichuana na Rais Emmanuel Macron katika uchaguzi wa uraisi wa Ufaransa kwa tikiti ya chama cha kitaifa cha Rassemblement chenye siasa kali za mrengo wa kulia ameeleza pia upinzani wake dhidi ya vazi la hijabu la wanawake wa Kiislamu.
Le Pen, alisema katika kampeni za uchaguzi huo kwamba iwapo atashinda kiti cha urais, atapiga marufuku kuchinja wanyama kwa njia ya Kiislamu na vilevile vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu.
3480733/