IQNA

Kadhia ya Palestina

Maeneo matakatifu ya Kiislamu na ya Kikristo huko Palestina 'Mstari Mwekundu': PA

18:55 - October 04, 2022
Habari ID: 3475876
TEHRAN (IQNA) - Mamlaka ya Palestina (PA) imeyataja maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo "mstari mwekundu".

Ofisi ya Rais ya Mamlaka ya Palestina amelaani mashambulizi ya mara kwa mara ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, mali zao na maeneo matakatifu chini ya ulinzi wa vikosi vinavyokalia kwa mabavu.

Nabil Abu Rudeineh, msemaji rasmi wa ofisi ya Rais ya Mamlaka ya Palestina, alisema katika taarifa yake: "Jeshi linalokaliwa kwa mabavu na walowezi wake wenye itikadi kali wanaendesha vita vikali kila siku dhidi ya miji, vijiji na kambi za wakimbizi za Palestina."

Abu Rudeineh alionya juu ya hatari ya miito ya wafuasi wa itikadi kali ya Kiyahudi ya kuvamiwa kwa kiwango kikubwa Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuvunjiwa heshima siku ya Alhamisi.

Amesisitiza kuwa "maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo ni mstari mwekundu, na hatutaruhusu madhara yoyote kuyapata hata kidogo."

Iwapo utawala wa Israel "ulitaka kukomesha ongezeko la hatari linaloendelea hivi sasa katika ardhi zote za Palestina, lazima uache jinai zake na ukomeshe mashambulizi ya walowezi."

Akihitimisha taarifa yake, Abu Rudeineh alisema kuwa uvamizi wa Israel "unatumia kimya cha kimataifa kuzidisha jinai na uchokozi wake dhidi ya watu wa Palestina katika jaribio la kunyonya damu ya Wapalestina wakati wa uchaguzi wa Israel."

3480725

captcha