IQNA

Fikra za Kiislamu

Idhini ya Qur'ani ya kujenga Misikiti katika kaburi la watu watukufu katika dini

21:15 - October 02, 2022
Habari ID: 3475871
TEHRAN (IQNA) – Aya ya 21 ya Surah Al-Kahf inabainisha kwamba kujenga msikiti katika makaburi ya watu watukufu na mawalii wa Mwenyezi Mungu sio tu inajuzu bali pia ni jambo ambalo inapendekezwa (Mustahabb).

Kuzuru makaburi watu watukufu na mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kitendo kinachokubalika katika madhehebu yote ya Kiislamu, hata katika Uwahabi. Hata hivyo, Mawahabi wanaamini kuwa mtu anapokufa kesi yake inafungwa na malipo ya matendo mema kama vile kusoma Qur'ani, kusaidia masikini, kujenga misikiti, shule n.k hayatamfikia. Wanaamini kuzuru makaburi inajuzu iwapo kutawakumbusha wageni wa Akhirah na kwamba wageni wanaweza tu kulilia dhambi zao wenyewe.

Hata hivyo, hii ni tofauti na yale Mtume Muhammad (SAW) na mafundisho ya Kiislamu yameonyesha. Mtume wa Uislamu aliwahi kusema mtu anayehiji Makka kisha akalizuru kaburi lake ni sawa na yule aliyekutana naye wakati wa uhai wake. Pia anasema mtu anayehiji Makka na kujiepusha kuzuru kaburi lake amemtendea vibaya.

Idhini ya  kujenga msikiti katika kaburi la watu watukufu na mawalii wa Mwenyezi Mungu

Kwa mujibu wa aya ya 21 ya Surah Al-Kahf, kujenga misikiti juu ya kaburi la sura za Mwenyezi Mungu haijuzu tu bali pia inapendekezwa. "Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao."

Katika aya hiyo, Mwenyezi Mungu SWT anasema amewakumbusha watu hadithi ya watu wa Kahf ili kuwapa moyo watu kuhusu Siku ya Kiyama. Watu walipoelewa hali ya wale watu saba, ambao walikuwa wamelala katika pango kwa miaka 300 hivi juu ya mapenzi ya Mungu, watu hao waaminifu walilala tena na kufa. Mzozo ulizuka miongoni mwa watu kuhusu nini cha kuwafanyia na hatimaye, wakaamua kujenga msikiti juu ya kaburi lao.

Makala hii ni sehemu ya matamshi yaliyotolewa na Ali Asghar Rezvani, mtafiti wa dini.

4088510

captcha