IQNA

Waislamu Uingereza

Misikiti ya Uingereza kupokea misaada ya kujikinga na wenye chuki

21:35 - May 21, 2022
Habari ID: 3475273
TEHRAN (IQNA)- Paundi milioni 24.5 zimetengwa kwa ajili ya usalama katika maeneo ya ibada na shule nchini Uingereza.

Misikiti na shule za Waislamu sasa zinaweza kutumia mfuko wa pauni milioni 24.5 (dola milioni 30.57) kwa ajili ya kuimarisha usalama.

Fedha hizo zinatolewa katika fremu ya ‘Mpango wa Kufadhili Ulinzi wa Maeneo ya Ibada’ ambayo yako katika hatari ya kukabiliwa na hujuma za wenye chuki.

Takwimu za uhalifu mwaka 2020/2021 zinaonyesha kuwa asilimia 45 ya uhalifu unaolenga wafuasi wa duni katika majimbo ya England na Wales nchini Uingereza ulikuwa ni dhidi ya Waislamu.

Waziri wa Usalama Uingereza Damian Hinds anasema: “Ni haki ya kimsingi kuweza kufuata mafundisho ya dini yako katika jamii.”

Amesema ufadhili huu kwa maeneo ya ibada ya Waislamu utasaidia kuzuia hujuma za wenye chuki na hivyo kufanya mitaa iwe salama zaidi.

Aidha amehimiza maeneo ya ibada ambayo yanahisi yako katika hatari ya kuhujumiwa na wenye chuki kujisajili kupokea misaada katika mfuko huo ‘Mpango wa Kufadhili Ulinzi wa Maeneo ya Ibada’.

Misaada hiyo itatolewa tu kwa maeneo ya ibada ya Waislamu na jamii za Waislamu zinaweza kuomba msaada wa kupata huduma za ulinzi na halikadhalika huduma kama vile kamera za usalama na ujenzi wa ua.

Mkuu wa  sirika la kutetea haki za Waislamu, Tell MAMA UK Iman Atta amekaribisha ubunifu huo wa serikali na kusema ni hatua ambayo itaimarisha usalma.

Uchunguzi wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu Uingereza umebaini kuwa asilimia 80 ya Waislamu Uingereza wanakabiliwa na chuki dhidi ya Uislamu.

Aidha takwimu rasmi za Uingereza zinaonyesha kuwa Waislamu ni jamii ya wachache inayokabiliwa na ubaguzi mkubwa zaidi. Takwimu zinaonyesha kuwa kuwa  ni vigumu kwa Waislamu kupata kazi ikilinganishwa na watu wa dini zingine.

3478985

captcha