Nakala 1000 tafsiri hiyo ya Kichina ya Qur'ani Tukufu zimechapishwa hivi karibuni na kusambazwa miongoni mwa Waislamu wa China.
Nakala asili ya tafsiri hiyo iko katika Jumba la Makumbusho la Taipei, mji mkuu wa Taiwan.
Tafsiri hii ya Qur'ani Tukufu iliandikwa na Hajj Abdul Rahman Ji Tuan na ina maelezo kuhusu baadhi ya aya.
Inaaminika kuwa Uislamu uliingia China katika karne ya saba Miladia ambapo Waislamu ni karibu asilimia 10 ya watu wote wa China. Baadhi ya takwimu zainaonyesha kuwa kuna Waislamu miliono 150 nchini China.