IQNA

Rais wa Ujerumani atuma salamu za Idul Fitr kwa Waislamu nchini humo

12:52 - May 24, 2020
Habari ID: 3472798
TEHRAN (IQNA) - Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idul-Fitr, ametaka wananchi wote washirikiane kwa ajili ya kuwalinda Waislamu wa nchi hiyo.

Rais Steinmeier ameyasema hayo kupitia ujumbe alioutoa kwa watu wa nchi hiyo na kusema kuwa, Ujerumani haiwezi kuvumilia chuki, mashambulizi na ukatili dhidi ya Waislamu na misikiti. Akisisitiza kwamba kulindwa Waislamu na misikiti yao nchini humo ni wadhifa wa raia wote, amewahakikishia wananchi kwamba binafsi anapambana na kila aina ya chuki na ubaguzi.

Kadhalika Rais Frank-Walter Steinmeier amewapongeza Waislamu wa nchi hiyo kwa kuzingatia na kuheshimu misingi ya kijamii na kidini katika mazingira ya sasa ya kuenea virusi hatari vya Corona. Hii ni katika hali ambayo Jumatano jioni rais huyo alikuwa mwenyeji wa chakula cha futari kilichoandaliwa katika ikulu ya rais wa Ujerumani. Kuenea virusi vya Corona kumeathiri amali za mwaka huu za mwezi wa Ramadhani na hata sherehe za Idul-Fitr kote duniani ambapo Waislamu wa Ujerumani pia walishiriki kwa kiwango kidogo sana katika swala za jamaa na mikusanyiko ya futari.

30301195

captcha