IQNA

Wananchi wa Iran washiriki katika Swala ya Idul Fitr + Video

12:24 - May 24, 2020
Habari ID: 3472797
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wameshiriki katika swala ya Idul Fitr baada ya kukamilisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Jana ofisi ya Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ilitoa taarifa na kusema, leo, Jumapili ni  tarehe Mosi Shawwal na siku kuu ya Idul Fitr baada ya mwezi kuandama.

Kwa mujibu wa maamuzi ya Idara ya Kitaifa ya Kupambana na COVID-19, kulikuwa na idhini ya kuswali swala ya Idul Fitr katika miji yote. Hata hivyo kwa mujibu wa maelekezo ya idara hiyo hakukuwa na swala katika viwanja vikubwa bali watu wamejimuika makundi madogo madogo katika misikiti na viwanja au mabustani mitaani ambapo waumini walioshiriki katika swala wamezingatia kanuni ya kutokaribiana na kuvaa barakoa. 

Kwa kawaida Swala ya Idi huswaliwa mjini Tehran katika Uwanja wa Swala wa Imam Khomeini  ambao una uwezo wa kubeba malaki ya waumini lakini mwaka huu kutokana na janga la COVID-19 wakuu wa afya nchini Iran wameshauri kuwa waumini wasijumuike katika eneo hilo. 

Leo katika aghalabu ya nchi za Kiislamu ni siku kuu ya Idul Fitr.

3471502

captcha