IQNA

Mashindano ya Qur’ani yafanyika Sweden kwa njia ya intaneti

18:17 - May 13, 2020
1
Habari ID: 3472763
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali AS mjini Stockholm, Sweden kimeandaa mashindano ya Qur’ani Tukufu kwa njia ya intaneti .

Taarifa ya kituo hicho imesema mashindano hayo yalianza tarehe 7 katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  na yataendelea hadi siku ya mwisho ya mwezi huu.

Washiriki wanaulizwa maswali kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram kila usiku na washindi wanatangazwa baadaye.

Mashindano hayo yanafanyika kila siku kuanzia saa moja usiku na washiriki wanapata fursa ya hadi saa kumi alasiri siku inayofuata kujibu maswali. Washindi wanapata  zawadi kama vile kitabu, tasbihi, marashi, zulia la kuswalia n.k. Washiriki kutoka nje ya Sweden wanaweza kushiriki lakini wakishinda zawadi zao zinaweza kutumwa tu ndani ya Sweden.

3898263

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Mwakimya
0
0
Ni hatua nzuri hii ya mashindano ya intaneti
captcha