IQNA

Wanajeshi wa Yemen watekeleza shambulizi jingine la ulipizaji kisasi uwanja wa ndege Saudia

14:49 - June 17, 2019
Habari ID: 3472005
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya Yemen vimetekeleza shambulizi jingine la ulipizaji kisasi kwa kuulenga uwanja wa ndege wa Abha, katika mkoa wa Asir kusini mwa Saudi Arabia. Shambulizi hilo limetekelezwa ikiwa ni katika kulipiza kisasi jinai dhidi ya Wayemen ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Saudia na waitifaki wake katika kipindi cha miaka minne sasa.

Kwa mujibu wa Televisehni ya Al Masirah, harakati ya Ansarullah  na waitifaki wake wameulenga kwa makombora uwanja wa ndege wa Abha Jumapili kwa kutumia drone au ndege isiyo na rubani aina ya Qasef K2. Uwanja wa ndege wa Abha uko karibu na kituo maarufu cha utalii katika eneo hilo la Saudi Arabia.

Siku ya Jumampsi pia vikosi vya Yemen viliushambulia wanja huo wa ndege wa Abha na uwanja mwingine katika mkoa jirani wa Jizan siku ya Jumapili kwa kutumia drone hiyo hiyo aina ya Qasef K2.

Jeshi la Yemen na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah Jumatano wiki iliyopita pia walivurumusha makombora dhidi ya uwanja wa ndege wa Abha huko kusini mwa Saudi Arabia na kuharibu mnara wa kuongozea ndege wa uwanja huo.

Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita jeshi na wapiganaji wa Yemen wametumia ndege zisizo na rubani kushambulia taasisi na vituo vya mafuta vya kampuni ya Aramco huko Saudi Arabia ambayo ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi duniani, jeshi hilo na wapiganaji wa Ansarullah pia wamedhibiti na kutwaa vituo zaidi ya 20 vya jeshi la Saudia huko Najran.

Tangu ulipoanzisha uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya Yemen mnamo mwezi Machi mwaka uliopita, hadi sasa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud na kuungwa mkono na Marekani umesha zishambulia skuli, hospitali, maeneo ya makaazi ya raia, barabara, masoko na kambi za wakimbizi na kuua maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Zaidi ya watu 10,000 wamepoteza maisha katika hujuma ya kinyama ya Saudia dhidi ya Yemen.

Lengo kuu la hujuma ya Saudia kuihujumu Yemen ni kumrejesha madarakani kibaraka wake, Rais mtoro wa nchi hiyo aliyejiuzulu Abd Rabu Mansour Hadi na kuwaondoa madarakani wanamapinduzi wa Ansarullah.

/3468761

captcha