Naibu Waziri wa Wakfu nchini Misri Mahmoud Bukhayt amesema mbali na shule hizo, pia vituo kadhaa vya kuhifadhi Qur'ani vimefunguliwa katika jimbo hilo.
Amesema gavana mpya wa El Wadi El Gedid ametoa wito wa kufunguliwa shule mpya za Qur'ani katika eneo hilo.
Aidha amesema serikali ya Misri inapanga kufungua shule mpya 150 za Qur'ani kote Misri.
Nchi ya Misri iko Afrika Kaskazini na idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 96 ambapo Waislamu ni asilimia 90 ya wakazi wa nchi hiyo.