IQNA

Jumba la Kitaifa la Makumbusho la Malek la Iran katika Fremu ya IQNA

Hajj Hussein Malek, alikuwa tajiri mkubwa mwenye raghba ya kutoa wakfu mbali na kuwa mpenda utamaduni na sanaa ya Iran. Aliasisi Maktaba na Jumba la Kitaifa la Makumbusho la Malke takribani mwaka 1900 katika mji Mtakatifu wa Mashhad. Baada ya kupita muda, vyote alivyokuwa amekusanya katika maktaba na jumba hilo la makumbusho alivichukua na kuvihamishia katika nyumba ya baba yake iliyokuwa katika Soko la Bein Haramein mjini Tehran ili wasomi na wanazuoni waweze kunufaika navyo. Baadaye mwaka 1937, aliandika barua rasmi na kukabidhi kila kitu alichokuwa nacho kwa Maktaba ya Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.

Jumba la Kitaifa la Makumbusho la Malek lina sarafu za kale, turathi za sanaa, mazulia, maandishi ya kaligrafia na nakala za kale na za kipekee za Qur'ani Tukufu.

Jengo la Jumba la Kitaifa la Makumbusho la Malek liko katika eneo al Meydan-e-Mashq (Medani ya Gwaride) mjini Tehran na kila siku idadi kubwa ya  maashiki wa utamaduni, sanaa na historia hutembelea eneo hilo.