IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran itafanikiwa kuvunja njama ya vikwazo na kutoa kipigo kingine kwa Marekani

19:44 - October 04, 2018
Habari ID: 3471701
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, majimui kubwa ya vijana wa nchi na taifa kubwa la Iran litaushinda wenzo wa mwisho wa adui yaani vikwazo na kutoa kipigo kingine dhidi ya Marekani.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika mjumuiko mkubwa na wa hamasa wa la jeshi la kujitolea la wananchi (Basij) katika Uwanja wa Azadi mjini Tehran ambapo sambamba na kubainisha kwamba, Marekani ikiwa na fikra zisizo sahihi imo mbioni kuunda taswira isiyo sahihi ya nguvu na uwezo wake na kuhusiana na hali ya mambo ya Iran na kuongeza kuwa, uchumi wa taifa la Iran unaweza kuvishinda vikwazo na kwa uwezo na tawfiki ya Mwenyezi Mungu tutavishinda vikwazo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kushindwa vikwazo hivyo kutakuwa na maana ya kushindwa Marekani na kwa msingi huo, Marekani itakuwa imechezea kipigo kingine kutoka kwa taifa la Iran.
Ayatullah Khamenei ameashiria kufedheheka 'demokrasia yya kiliberali' ya Marekani na kuenea kukosolewa kwake duniani na kueleza kwamba, ni kwa sababu hiyo ndio maana licha ya Marekani kuwa na nguvu ya atomiki, teknolojia ya hali ya juu na uwezo mkubwa wa kifedha, lakini imeshindwa katika maeneo mengi kama huko Iraq, Syria, Lebanon, Pakistan na Afghanistan na kuna vipigo vingine vinavyoisubiria Washington.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, kuokoka Iran kutoka katika ubeberu wa kidhulma wa Uingereza na Marekani kunatosha kuthibitisha nguvu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, kutoshindwa taifa la Iran chimbuko lake ni baraka za Uislamu na huku kutoshindwa kunaweza kushuhudiwa katika ushindi wa taifa hili katika Mapinduzi ya Kiislamu, kutetea matukufu na kusimama kidete dhidi ya njama zote dhidi yake katika kipindi chote hiki cha miaka 40 ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

3752700

captcha