IQNA

Kiongozi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin Misri afungwa maisha jela

21:55 - September 23, 2018
Habari ID: 3471687
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa kundi la Ikhwanul Muslimin la Misri na makumi ya wananchama wa kundi hilo wamehukumiwa kifungo cha maisha jela .

Kwa mujibu wa taarifay hukumu iliyotolewa mahakama ya mji wa Minya inayosema kuwa, Mohammed Badie, mkuu wa Ikhwanul Muslimin na wanachama wengine 64 wa kundi hilo wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za kuhusika katika machafuko yaliyotokea katika mji wa el Idwa, mkoani al Mania tarehe 14 Agosti 2013.
Hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Mohammed Badie imetolewa katika hali ambavyo hivi karibuni pia mahakama ya rufaa ya Cairo ilimuhukumu kifungo cha maisha jela kwa kumuhusisha na kesi ya mgomo na kukusanyika wafuasi wa Mohamed Morsi katika medani za ,Rabia al Adawiya na al Nahdha mjini humo baada ya rais huyo wa zamani wa Misri kupinduliwa na jeshi mwaka 2013.
Vile vile mahakama ya rufaa ya Cairo imewahukumu kifo wafuasi wengine 75 wa Ikhwanul Muslimin kwa kuhusika na machafuko ya mwaka 2013 na kuwahukumu wafuasi wengine 46 wa kundi hilo kifungo cha maisha jela.
Tarehe 14 Agosti 2013, rais wa hivi sasa wa Misri, Abdel Fattah el Sisi ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wakati huo, alitoa amri ya kushambuliwa wafuasi wa Mohamed Morsi mjini Cairo na kuua na kujeruhi mamia ya watu.
Mwaka 2013, viongozi wa Misri waliiweka Ikhwanul Muslimin katika orodha ya makundi ya kigaidi na wamekuwa wakichukua hatua kali dhidi ya wafuasi wa kundi hilo.
Kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Julai mwaka 2013, Mohammad Morsi aliondolewa madakarani na huo ukawa mwanzo wa kipindi kingine cha masaibu ya Ikhwanul Muslimin.
Rais Abdel Fatah El Sisi wa Misri anasisistiza kuhusu kukandamizwa Ikhwanul Muslimin kwa visingizio kama vile kuhusika harakati hiyo na vitendo vya misimamo mikali ya kidini. Ukandamizaji huo utapalekea mgogoro kuibuka Misri na mgawanyiko katika jamii na hivyo kuifanya kazi ya El Sisi kuwa ngumu zaidi. Njia pekee ya Misri kujikwamua katika mgogoro uliopo ni kuwepo maelewano katika uga wa kisiasa nchini humo ili taifa hilo la Afrika Kaskazini liweze kustawi na kufikia malengo ya juu ya mapinduzi ya wananchi ya mwaka 2011 ambayo yalipelekea kuondoelwa madarakani diketeta Husni Mubarak ambaye aliitawala nchi hiyo kwa miongo mitatu.

3749372

captcha