IQNA

Wanachuo 200 waliohifadhi Qur’ani wahitimu chuo kikuu Nigeria

16:43 - July 31, 2018
Habari ID: 3471614
TEHRAN (IQNA)- Wanachuo zaidi ya 200 waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu wamehitimu katika Kituo cha Masomo ya Qur’ani cha Chuo Kikuu cha Bayero cha Jimbo la Kano (BUK).

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika sherehe iliyofanyika Jumamosi, mkurugenzi wa kituo  hicho Dr Muhammad Babangida amesema waliohitimu, mbali na mafunzo ya Qur’ani, pia wamepata mafunzo ya sayansi ya kompyuta, hisabati na lugha ya Kiingereza.

Amesema wanafunzo hao wamepata  ya kiwango cha juu na kwa vyeti walivyonavyo wanaweza kufunza Qur’ani katika nchi zote za Kiislamu duniani.

Aidha ametoa wito kwa wanachuo waliohitimu, ambao ni maarufu kama Alarammomi nchini Nigeria’ kutumia ujuzi waliopata kuimarisha maisha yao kijamii na kiuchumi.

Naibu mkuu wa chuo hicho Profesa Muhammad Bello naye ametoa wito kwa serkali za majimbo ya nchi hiyo kuwaajiri waliohitimu katika shule za umma ili kuongeza idadi ya waliohifadhi Qur’ani nchini humo.

3466427

captcha