IQNA

Mwalimu aliyevunjia heshima Qur'ani ashtakiwa Kenya

13:43 - July 30, 2018
Habari ID: 3471612
TEHRAN (IQNA)- Mwalimu mmoja aliyeivuinjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Kenya katika eneo la kaskazini mashariki anatazmaiwa kufikishwa kizimbani.

Polisi katika eneo bunge la Ijara, Kaunti ya Garissa wamemkamata mwalimu hiyo ambaye aliukanyaga msahafu wakati alipokuwa akifundisha somo la Kiingereza hivi karibuni.

Akipatikana na hatia, mwalimu huyo atafungwa miaka mitanto jela kwa kuvunjia heshima mtukufu ya kidini. Ingawa Kenya haina sheria maalumu ya kuvunjia heshima matukufu ya kidini, lakini polisi wamesema watatumia kipengee maalumu kumshtaki mwalimu.

Mwalimu huyo asiyekuwa Mwislamu ambaye jina lake halikutajwa alitenda kitendo hicho Jumatano iliyopita katika Shule ya Taqwa Academy katika mji wa Masalani. Wazazi waliokuwa na hasira walivamia shule hiyo wakitaka kumchoma mwalimu huyo kabla ya maafisa wa polisi kuingilia kati na kumakamata. Siku ya Ijumaa maimamu 42 kutoka misikiti ya eneo hilo waliandamana walitaka mwalimu huyo atimuliwe kutoka eneo hilo.

3466436

captcha