IQNA

Wafungwa Waislamu Marekani walishwa nyama ya nguruwe mwezi wa Ramadhani

19:13 - May 25, 2018
Habari ID: 3471530
TEHRAN (IQNA)-Baraza La Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limewasilisha malalamiko mahakamani baada ya kubainika kuwa wafungwa katika jimbo la Alaska wanalishwa nyama ya nguruwe katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya Alhamisi CAIR ilifanikiwa kupata hukumu ya jaji wa Mahakama ya Federali ambaye ametaka wakuu wa Gereza la Anchorage kuacha kuwapa wafungwa Waislamu nyama ya nugurwe.

Katika taarifa, CAIR imesema gereza hilo limekiuka taratibu za magereza na katiba kwa kuwalisha Waislamu nyama ambayo imeharamishwa kwa mujibu wa mafundishyo ya Uislamu.

Waislamu katika mji wa Anchorage jimboni Alaska wanafunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa masaa 18 ambapo mbali na kulazimishwa kula nyama ya nguruwe pia wanapewa lishe duni sana wakati wa  futari na daku. CAIR imesema katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani Waislamu wanapewa mlo wenye kalori 1,100 kwa siku ambao ni chini ya kiwango cha kila siku  kilichopendekezwa na wataalamu cha kalori 2,500 kwa wanaume.

CAIR inasema tokea Donald Trump achaguliwe kuwa rais wa Marekani, Waislamu nchini humo wameshuhudia ongezeko kubwa la ubaguzi dhidi yao huku wakishambuliwa na kubugudhiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

3465926

captcha