IQNA

Mkutano wa changamoto za jamii za Waislamu waliowachache duniani

16:55 - May 10, 2018
Habari ID: 3471504
TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa kimataifa wa kujadili changamoto za jamii za Waislamu waliowachache katika nchi zisizo za Kiislamu umefanyika.

Kongamano la Kimataifa la Jamii za Waislamu Wachache limefanyika Jumanne mjini Abu Dhabi katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE,  na kuwaleta pamoja wajumbe 550 waliojumuisha viongozi wa kisiasa, kidini na kielimu. Washiriki wamejadili njia za kukabiliana na changamoto zinazowakabilia Waislamu milioni 500 wanaoishu kama jamii za wachache katika nchi zisizo za Kiislamu. Kikao hichyo aidha kimewachimiza Waislamu kuishi kwa amani na maelewano na watui wasiokuwa Waislamu. Maudhui nyingine muhimu katika kikao hicho ilikuwa ni kuhusu mbinu za kukabiliana na chuki dhidi ya Waislamu.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Waziri wa Stahamala UAE Sheikh Nahyan bin Mubarak ameuhutubu katika kikao hicho na kusema nchi yake ni mfano mwema wa kuigwa katika suala la jamii mbali mbali kustahamiliana. Amesema nchi yake inategemea mafundisho ya Uislamu katika kueneza amani na ustawi na maelewano.

Viongozi wa jamii za Waislamu wametoa wito kwa Waislamu kuheshimu na kutii sheria za nchi wanazoishi na kuishi kwa amani na wenzao.

3712745

captcha