IQNA

Wapalestina 54 wafariki baada ya Israel kuwanyima vibali vya matibabu

10:41 - February 15, 2018
Habari ID: 3471392
TEHRAN (IQNA)-Wapalestina wasiopungua 54 walipoteza maisha mwaka 2017 baada ya utawala haramu wa Israel kuwanyima vibali vya kupata matibabu nje ya eneo lililochini ya mzingiro la Ukanda wa Ghaza.

Katika taarifa ya Jumanne ya Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu cha Al Mezani cha Ghaza, kwa ushirikiano na taasisi kadhaa za kimataifa, Wapalestina hao waliofariki walikuwa miongoni mwa mamia ambao utawala wa Kizayuni wa Israel uliwanyima vibali vya kuondoka Ghaza kuenda kupata matibabi nje ya eneo hilo.

Taarifa zinasam mwaka 2017, Israel iliidhinisha nusu ya maombi ya vibali vya tipa kutoka kwa Wapalestina na hivyo kusababisha vifo na masaibu kwa Wapalestina katika eneo hilo ambalo hospitali zake hazina suhula kutokana na mzingiro uliowekwa na utawala huo wa Kizayuni.

Tokea mwaka 2007, utawala haramu wa Israel uliweka mzingira wa anga, nchi kavu na baharini dhidi ya Ukanda wa Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuichagua kidemokrasia harakati ya Hamas kuongeza eneo hilo. Mzingiro huo umelifanya eneo hilo lenye watu karibu milioni moja na nusu kutajwa kuwa gereza kubwa zaidi la wazi duniani. Misri inashirikiana na Israel katika kuwawekea Wapalestina mzingiro kwani njia ya nchi kavu inayounganihsa Ghaza na nchi zingine duniani ni kupitia mipaka ya Misri.

Mbali na mzingiro huo, utawala haramu wa Israel pia umeanzisha vita mara tatu dhidi ya Ghaza tokea mwaka 2008 ambapo maelfu ya Wapalestina wakiwemo wanawake na watoto wameuawa mbali na miundo mbinuya eneo hilo kama vile mahospitali, shule na nyuma za makazi kuharibiwa.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitahadharisha Jumatatu ya jana kwamba, kwa mujibu wa utafiti wa umoja huo ni kuwa, kufikia mwaka 2020 eneo la Ukanda wa Gaza halitafaa kwa ajili ya kuishi.

Antonio Guterres amesema kuwa, hali ya kibinadamu na kiuchumi ya Ukanda wa Gaza ni mbaya mno. Ameongeza kuwa, eneo la Ukanda wa Gaza lingali linataabika kwa mgogoro wa binadamu kutokana na kufungwa vivuko vya kuelekea katika eneo hilo.

3465186

captcha