IQNA

Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan

Qur'ani Tukufu ni Ramani ya Nji katika Maisha ya mwanadamu

11:10 - January 28, 2018
Habari ID: 3471374
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan Ahsan Iqbal amesema Qur'ani Tukufu ni kama ramani ya njia katika mwaisha ya mwanadamu.

Akizungumza katika sherehe ya mwaka wa 20 wa kuasisiwa Sout-ul-Qur'ani katika Kituo cha Utangazaji cha Pakistan, Iqbal ameongeza kuwa, kusoma kwa kina na kufahamu ipasavyo mafundisho ya Qur'ani Tukufu ni nukta zinazoweza kumsaidia mwanadamu kufikia upeo mpya wa sayansi na teknolojia.

Ameongeza kuwa, Qur'ani Tukufu inamtaka mwanadamu afanye utafiti na uchunguzi kuhusu maumbile ya ulimmwengu na mfumo mzima wa sayari. Hatahivyo amebainisha masikitiko yake kuwa, Waislamu hawajafaidika na aya za Qur'ani Tukufu. "Tukiwa kama Waislamu ni jukumu letu kufanya utafiti wa kina kuhusu Qur'ani Tukufu ili tufaidike maumbile ya ulimwengu."

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Pakistan amesema Sout-ul-Quran inawahudumia watu wa matabaka yote ya jamii na kuwawezesha kusikiliza tafsiri za Qur'ani kwa masaa 19 kila siku kutoka katika vituo 19 katika maeneo mbali mbali nchini humo.

Amesema serikali inafanya mpango wa kuhakikisha idhaa hiyo ya Qur'ani inawafikia watu wote nchini humo hiyo kwa njia ya FM.

3465052

captcha