IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wenye ulemavu wa macho kufanyika Iran

19:30 - January 31, 2018
Habari ID: 3471358
TEHRAN (IQNA)-Duru ya Tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wenye Ulemavu wa Macho imepangwa kufanyika hapa nchini Iran mwezi Aprili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ya Qur'ani ya wenye ulemavu wa macho yatafanyika kati ya Aprili 19-26 mjini Tehran sambamba na Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

Kati ya masharti ya kushiriki katika mashindano hayo ni kuwa mshiriki asiwe alishiriki katika mashindano ya mwaka jana. Aidha wanaoshiriki wanapaswa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45 na wawe na uwezo wa kusoma Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia kanuni na misingi yote ya tajwid, saut na lahn.

Halikadhalika kila mshiriki anaruhusiwa tu kuandamana na mtu moja ambaye atamsaidia ambapo gharama zote za usafairi, makazi na malazi zitasimamiwa na wenye kuandaa mashindano.

Walio na azma ya kushiriki katika mashindano hayo wanahitaji kutuma kopi ya pasi ya kusafiria, picha mbili za paspoti na kujaza fomu ya washiriki na kuiwasilisha kabla ya tarehe 7 Februari 2018 sawa na 18 Jamadu Thani 1439 Hijria Qamaria.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mashindano hayo ya Qur'ani kwa kubonyeza hapa au kupitia barua pepe au email ambayo ni awqafiran@vahoo.com , nambari ya simu 00989223784093 na nambari ya Faxi ni 009821-64872627. Halikadhalika unaweza kuwasiliana na wasimamizi wa mashindano kupitia mitandao ya kijami katika @awqafiran na +989223784093.

3683142

captcha