IQNA

Harakati ya Ansarullah ya Yemen yavurumisha kombora Abu Dhabi, UAE

20:40 - December 03, 2017
Habari ID: 3471293
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Ansarullah ya Yemen imevurumisha kwa mafanikio kombora la Cruz na kulenga Abu-Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ikiwa ni jibu kwa jinai UAE dhidi ya watu wa Yemen

Harakati ya Ansarullah ya Yemen yavurumisha kombora Abu Dhabi, UAEWapiganaji wa Yemen leo Jumapili asubuhi walirusha kombora aina ya Cruz katika kituo cha nguvu za nyuklia cha Baraka kilichopo Abu-Dhabi mji mkuu wa Imarati. Saifullah al Shami ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa na Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kuwa vikosi vya kujitolea vya nchi hiyo vimetangaza mara kadhaa kwamba vina makombora yenye uwezo wa kuipiga miji yote mikuu ya nchi adui.

Al Shami amebainisha kuwa kombora lililovurumishwa kuelekea Abu-Dhabi linaonyesha kuwa vitisho na mashinikizo ya audi dhidi ya taifa la Yemen havina maana. Kombora lililovurumishwa na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen katika kituo cha nguvu za nyuklia huko Abu-Dhabi ni la aina ya Cruz lenye uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 1200.

Tangu mwezi Machi mwaka 2015, Saudia, ikisaidiwa na kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa UAE na Marekani ilianzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Yemen kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi.

Raia zaidi ya elfu 13 wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia tokea mwezi Aprili mwaka huu.

Halikadhalika kutokana na hujuma hiyo ya Saudia na UAE dhidi ya Yemen, Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 20 kati ya jamii ya watu milioni 25 ya Yemen wanahitajia misaada ya kibinadamu.

3669236

captcha