IQNA

Maimamu barani Ulaya wasisitiza kuhusu ujumbe wa amani katika Qur’ani

21:19 - November 27, 2017
Habari ID: 3471284
TEHRAN (IQNA)- Maimamu na wahubiri wa Kiislamu barani Ulaya wameshiriki katika mkutano wa siku moja mjini Brussels Ubelgiji kwa kusisitiza kuhusu ujumbe wa amani wa Qur’ani Tukufu kwa wanadamu wote.
Maimamu barani Ulaya wasisitiza kuhusu ujumbe wa amani katika Qur’ani"Ujumbe mkuu katika kongamano la leo ni kuwa, Qur’ani Tukufu inasisitiza kuhusu utamaduni wa amani,” alisema Sheikh Khalid Hajji, mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa Wamorocco Barani Ualaya ambalo liliandaa kongamano hilo.

Amesema Qur’ani Tukufu imeibua ustaarabu ambao umewawezesha wanadamu kuishi pamoja kwa amani. "Qur’ani Tukufu inaweza kuchangia katika kutuwezesha kufahamu maana ya maisha katika utamaduni wa sasa wa kidijitali,” amesema Sheikh Hajji.

Mwanazuoni huyo kutoka Morocco amesema kuwa, Qur’ani Tukufu inawataka Waislamu watafakari na iwapo agizo hilo litafuatwa basi Waislamu katika nchi za Magharibi wanaweza kuboresha uhusiano wao na jamii wanamoishi.

Kikao hicho kilimalizika kwa kikao cha qiraa ya Qur’ani Tukufu kilichowajumuisha wasomaji 14 kutoka nchi mbali mbali za Ulaya.

3464517

captcha