IQNA

Utawala wa Kiimla Saudia walenga kuwanyamazisha Waislamu wa Kishia kwa kuwanyonga

10:45 - July 14, 2017
1
Habari ID: 3471065
TEHRAN (IQNA)- Katika kuendelea ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia, utawala wa Aal Saud umewanyonga raia wanne wa nchi hiyo wa mji wa Qatif.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, watu wanne ambao ni wakazi wa mji wa Qatif walinyongwa juzi Jumanne kwa tuhuma za kushiriki katika operesheni ya kigaidi. Viongozi wa Saudia wamekuwa wakitumia suala la ugaidi kwa ajili ya kutekeleza baadhi ya sheria ngumu na adhabu kali dhidi ya raia wa nchi hiyo wanaopigania haki yao ya uhuru wa kutoa maoni na wale wanaofanya maandamano ya amani yenye madai kwa utawala wa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo, Mahakama ya Rufaa ya Saudia imeidhinisha hukumu ya kunyongwa kijana mmoja wa Kishia wa nchi hiyo ambaye amekuwa akishikiliwa kizuizini tangu mwaka 2014 na kukabiliwa na mateso makubwa akiwa korokoroni. Saudia imekuwa ikitumia mbinu ya kutekeleza hukumu ya kifo na vifungo vya muda mrefu jela kama njia ya kukabiliana na wimbi la ukosoaji la asasi za haki za binadamu likiwemo Shirika la haki za Binadamu la Human Rights Watch na Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International.

Siasa za utumiaji mabavu

Ni karibu miaka miwili na nusu sasa tangu utawala wa Aal Saud ulipopasisha sheria inayodaiwa kuwa ni ya "Kupambana na Ugaidi' na kwa msingi huo kuongeza vitendo vya ukiukaji wake wa haki za binadamu dhidi ya raia wa nchi hiyo. Ukweli wa mambo ni kuwa, hatua hiyo ya Saudia inalenga kuhalalisha ukandamizaji inaoufanya dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Kwa hakika matukio ya nchini Saudia yanaonyesha kushadidi siasa za utumiaji mabavu na kunyongwa wapinzani tangu Mfalme Salman alipochukua hatua za uongozi wa nchi. Inaelezwa kuwa, Januari mwaka jana Saudia ilikuwa nchi ya kwanza katika historia kufanya unyongaji wa umati. Ikumbukwe kuwa, Januari Pili mwaka jana, Saudia iliwanyonga kwa umati wafungwa 57 akiwemo Sheikh Nimr Baqir al-Nimr mwanazuoni mwanamapambano wa nchi hiyo.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, chimbuko la kushadidi vitendo vya kufurutu ada vya utawala wa Aal Saud katika miaka ya hivi karibuni iwe ni katika masuala ya ndani au katika siasa zake za nje ni kuzidi kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo Mawahabi.Jambo hili linashuhudiwa zaidi katika kipindi cha Mfalme Salman.

Nafasi ya Uwahabi katika kukandmizwa Mashia

Katika muendelezo wa kuwafuta kazi na kuwateua maafisa wapya, hivi karibuni Mfalme Salman aliwateuwa washauri wake maalumu wanne wawili wakiwa wanatoka katika familia ya Aal Sheikh ambayo inanasibishwa na Muhammad bin Abdul-Wahhab mwasisi wa kundi lililopotea la Uwahabi. Katika majuma ya hivi karibuni wimbi kubwa la mabadiliko katika uga wa siasa za Saudia linaonekana kutanda zaidi ambapo kunashuhudiwa hatua za Mfalme Salman za kutaka kudhibiti mamlaka yote ya nchi hiyo upande wa Uwahabi na kuwa na muelekeo wa kimakundi.

Sambamba na hatua hizo, kunaonekana kushadidi hatua zisizo na vipimo wala hekima ambazo ni za kufurutu ada za Saudia za kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine kieneo na kimataifa. Huku hayo yakijiri Saudia imeendelea kukabiliwa na changanmoto mbalimbali za ndani likiwemo suala la vita vya kuwania madaraka ndani ya familia ya Aal Saud.

Si hayo tu, hakuna wakati ambao utawala huo ulipata uhalali na ridhaa ya kutosha ya wananchi wa Saudia. Moja ya sababu za utawala huo kukumbwa na hatima hiyo ni kwamba, familia ya Aal Saud kutokana na kuathirika na mafundisho potovu ya Kiwahabi imekuwa haina imani kabisa na suala zima la haki za raia, haki za binadamu na demokrasia.

Kushadidisha Saudia ukandamizaji dhidi ya matabaka mbalimbali ya wananchi wakiwemo Waislamu wa Kishia kumeifanya nchi hiyo kuhesabiwa kuwa moja ya mataifa yanayokiuka pakubwa haki za binadamu ulimwenguni.

3463345

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Ngabo Ibrahim
0
0
Hebu, jamani, tutabaki tunapiga tu kelele na huku tunauliwa kanakwamba sisi sio wanadamu. Basi kwa nini hatuunde kikosi
Na kuwa piganisha ili kuikomboa ardhi ya suudiyya?
captcha