IQNA

Zawadi ya Mustafa SAW

Iran yawatunuku zawadi wanasayansi bora Waislamu

19:54 - December 26, 2015
Habari ID: 3469674
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanzisha Zawadi ya Kimataifa ya Mustafa (SAW) ambapo imewatunuku zawadi wanasayansi bora zaidi Waislamu duniani katika hafla iliyofanyika Tehran.

Omar Yaghi wa Jordan na Jackie Yi-Ru Ying kutoka Singapore wametunukiwa zawadi za katika Hafla ya Kwanza ya Zawadi ya Mustafa SAW. Wanayasanayo hao wamepataza zawadi katika nyuga za bioteknolojia, tiba na nanoteknolojia. Ying alizaliwa mwaka 1966 ni ni mtaalamu wa nanoteknolojia na mkurugenzi wa Taasisi ya Uhandisibio na Nanoteknolojia nchini Singapore. Amevumbua dawa inayosaidia watu wenye ugonjwa wa kisukari. Akizungumza wakati wa kutunukiwa zawadi hapa Tehran, alisema zawadi hiyo iliyoanzishwa na Iran itatoa mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha sanaysi na teknolojia katika ulimwengu wa Kiislamu.
Nayo Omar Yaghi ambaye amechaguliwa kwa ajili ya utafiti wake katika nanoteknolojia ya metal-organic frameworks (MOFs) amewashukuru waandalishi na kusema ni fahari yake kuwa kupokea tuzo hiyo.
Akizgungmza katika kikao hicho Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya Sayansi na Teknolojia Sorena Sattari amesema Zawadi ya Mustafa SAW inalenga kuhuisha nafasi ya uongozi wa utaarabu wa Kiislamu katika sayansi na teknoolojia. Amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa mstari wa mbele katikaa utumizi wa kibinadamu wa sayansi na teknolojia ili kuimarisha misingi ya amani, maisha bora, usalama na afya ya wanadamu wote. Ameelezea matumaini kuwa zawadi hiyo itapelekea kuimarika ushirikiano baina ya wanasayansi na wasomi duniani kote. Zawadi ya Mustafa SAW ni zawadi ya chuu zaidi ya sayansi na teknolojia ambayo hutunukiwa wanasayansi na watafiti na watafiti bora zaidi wa nchi za Kiislamu duniani. Washindi wa Zawadi ya Mustafa SAW hupata zawadi ya nusu milioni dola pamoja na vyeti.

3469187

captcha